fisa mtendaji wa kijiji cha Dulamo amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jera ama kulipa faini ya sh. laki tano kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa ya sh.laki tano ili asimfikishe polisi mzazi ambaye alikuwa akimuozesha mwanafunzi.
Hukumu hiyo ilitolewa Mei 17 katika mahakama ya Wilaya ya Njombe Mkoani Iringa Mbele ya hakimu mfawidhi Bw. Fredrick Lukuna,ambaye alikuwa akisiliza kesi hiyo.
Akisoma shitaka lililokuwa likimkabili Ofisa mtendaji huyo Bw.Fidelisi Mwajembe, mendesha mashtaka kutoka kitengo cha kuzuia na kupambana na rushwa Wilayani hu mo (TAKUKURU) Bw.Richard Malekano alisema mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa kwa kushirikiana na Ofisa mtendaji wa kata ya Usuka Bi Upendo Fute ambaye mahakama ilimwachia huru baada ya kukutwa hana hatia walitenda kosa hilo Novemba 19 2009.
Bw.Malekano alisema watuhumiwa hao wakiwa watumishi wa serikali ngazi ya kata na kijiji walishawishi na kuomba rushwa kutoka kwa Bi.Edina Mwalongo ambaye alikutwa akimuoza mwanafunzi aliyefahamika kwa jina la Felista lukenda ili wamalize kesi kinyenyeji pasipo kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Ilidaiwa kuwa Bi. mwilongo kwa kuhofia kufikishwa katika sheria alikubali kutoa fedha hizo ambazo hata hivyo alikopa na kufanikiwa kutoa kiasi cha sh. 260,000, badala ya sh. 500,000, ambazo aliombwa na watuhumiwa hao, ambapo alitoa taarifa kwa barozi juu kile kilichotokea na kufanikiwa kuwatia hatiani watuhumiwa kwa pamoja.
Kama haitoshi watuhumiwa hao walidaiwa kuwa baada ya kufanikiwa kuchukua fedha hizo kutoka kwa Bi. Mwilongo pia walichukua kiasi cha sh. 70.000 kutoka kwa ndugu wa mtuhumiwa Bi. Juliana Mwinuka ambazo hata hivyo walikanusha na kudai kuwa fedha hizo zilikuwa adhabu kwa kosa la kuoa mwanafunzi na kwamba fedha hizo zilitumika kununua mifuko ya ssruji katika shule ya Chalowe ambako alikuwa akisoma mwanafunzi huyo.
Hata hivyo mahakama ilimwachia huru B. Fute baada ya ushahidi uiliotolewa mahakamani hapo na kuonekana kuwa mwenye hatia alikuwa ni Bw. Mwajombe kwani ndiye aliyekuwa akipokea fedha kutoka kwa ndugu wa mwoaji na muaozaji, hata hivyo Bi. Fute anakabiliwa na shitaka jingine la kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa mganga wa jadi aliyekuwa anatuhumiwa kwa kosa la kumpa mwanamke mmoja dawa ya kutoa ujauzito ambapo hukumu ya kesi hiyo itasomwa Mei 30 katika mahakama hiyo.
Baada ya mshtakiwa kupewa nafasi ya kujitetea Bw. Lukuna alisema anatoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwa watu wengine ambao kwa namna moja ama nyingine wana nia ya kutaka kufanya kosa kama hilo.