Karibu katika Blogu hii ya Siwale!

ELIMU

Sekta ya elimu wilaya ya Mbarali mkoani mbeya imezidi kushuka kitaifa kutoka asilimia 70.5 mwaka 2006 hadi kufikia asilimia 49.4 mwaka jana 2009.




Afisa elimu wa sekondari wilaya ya Mbarali Bw.Gaddy tende amesema hayo wakati wa mkutano wa dharula ulioitishwa na mwenyekiti wa halmashauri hiyo Bw.Keneth Ndingo,kufuatia taluma kuzidi kudidimia mwaka hadi mwaka.



Bw.Tende amesema tayari utafiti umebaini kuwa yapo mabo zaidi ya 29 yanayochangia kuportomika kwa elimu kila mwaka ambayo yanafanyiwa mkakati ili kuikabili changamoto hiyo inayooneka na kushusha taaluma.



Amesema kati ya changamoto hizo zilizobainishwa na wadau ni utoro wa walimu katika vituo vya kazi ,mahusiano hafifu kati ya uongozi wa elimu wilaya ,waratibu elimu kata na wakuu nwa shule kiutendaji.



Ambapo rasimu mpya ya maamuzi ya wadau hao itashughulikia pia changamoto za ukosefu wa nyumba za kuishi walimu ,ufundishaji usiozingatia taaluma kwa mwalimu kufundisha somo la kiingereza kwa Kiswahili pamoja na uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi ,kiingereza na hisabati.



Aidha mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Bw,Ndingo amesema sekta ya elimu imeshuka kupitia wizara husika kubadili mara kwa mara mitaala na silabasi za kufundishia masomo ya muda wa ziada ,mitihani ya kujipima ya kata ,wilaya na shule ambayo inachukua nafasi za masomo rasmi na wanafunzi kujifunza mambo yasiyo husiana na mitahani inayotolewa kitaifa.



MWISHO.