Uovu mwingine wa utekaji nyara watoto umezuka katika wilaya ya mbozi mkoani mbeya ,huku wahalifu hao wakidai waingiziwe fedha kwenye akaunti na wazazi ili kunusuru maisha ya watoto wao .
Mkoa wa mbeya hususan wilaya za mbozi .ileje na rungwe umekuwa na matukio ya mauaji ya kutisha kama vile uchunaji ngozi ,mauaji ya watoto na sasa utekaji wa watoto wadogo kwa lengo la wahusika kujipatia fedha isivyo halali.
Tukio mla hivi karibuni mototo Bonifasi Mahenge(7) alitekwa akiwa shuleni eneo la ichenjezya Vwawa wilayani mbozi ,ambapo wahusika walipiga simu ya na kuandika ujumbe mfupi (SMS)kwa baba mlezi wa motto Bw.Exaud Kajela kumtaka awape Sh. 500,000/= LAKI TANO.
Bw. Kajela ,alisema ili kuokoa masha ya mototo wake alikubali kuweka fedha katika akaunti aliyotakiwa kuingiza benki ya NMB tawi la Vwawa kiasi cha Sh.300.000/= laki tatu,ambazo ambazo zilichukuliwa muda mfupi na wahusika kabla ya kutiwa mbaroni.
Kamanda wa polisi mkoani Mbeya ,kamishna wa polisi Advocate Nyombi,amewataja watuhumiwa wa tukio hilo kuwa ni Bw.Martini Mwarwanda na dada yake Bi.Hawa Mwarwanda mtuhumiwa wa tatu jina lake limehifadhiwa wakati akisaidia upelelezi wa tukio hilo.
Kamanda Nyombi ametoa wito kwa wananchi kukomesha uovu huo kwa kutoa ushirikiano kwa viongozi wa eneo husika na dhana nzima ya polisi jamii kuitumia na kuwataka kila mtu kuwa mlinzi wa mwingine sanjari na kuzuia ama kukomesha kabisa uhalifu.
MWISHO.