Karibu katika Blogu hii ya Siwale!

Mbeya





WATU watatu wanashikiliwa na jeshi la polisi Mkoani Mbeya kwa matukio mawili tofauti ya utekaji wa watoto ili kujipatia pes kwa njia isiyokuwa halali katika Wilaya ya Mbozi na Mbeya Mjini.



Katika tukio la kwanza lililotokea Mei 13 wilayani Mbozi katika kijiji cha Ichenjezya, kamanda wa polisi kamishina msaidizi Bw. Advocate Nyimbi alisema, mtoto Bonface Mahenge (7) alitekwa na watu wakati alipokuwa akielekea shuleni.



Bw. Nyombi alisema watekaji hao baada ya kufanikiwa kumteka mtoto huyo walimpigia simu mlezi wa mtoto huyo ambaye alifahamika kwa jina la Bw. Exude Kajela mkazi wa kijiji cha Ichenjezya na kumtaka aweke pesa benki katika akaunti ya benki ya NMB kwa namba ambazo alimtajia ndipo arudishiwe mtoto na kumtishia endapo hatafuata maelekezo aliyopewa uhai wa mtoto huyo ulikuwa mikononi mwao.



Alisema baada ya kupewa namba za akaunti alizotakiwa kuweka pesa , Bw. Kajela alitoa taarifa polisi na kwamba alitekeleza na kuweka kiasi cha fedha shilingi laki tatu badala ya tano ambazo mtekaji alizihitaji, ambapo baada ya kufanya hivyo alipigiwa simu kwa namba tofauti na kuambiwa kuwa mtoto wako utamkuta katika kituo cha mafuta cha Gapco kilichopo kijijini hapo.



Bw. Nyombi alieleza kuwa, Bw. Kajela baada ya kupigiwa simu hiyo na kuelekezwa mtoto alipo alirudi kwa meneja wa benki na kuomba kuangalia ikiwa pesa zilizowekwa katika akaunti hiyo zipo ama zimechukuliwa, jambo ambalo liliwashangaza ni kwamba pesa hizo zilionekana zimechukuliwa muda mfupi badaaba ya kuwekwa hali ambayo ilionesha watekaji hao walikuwa karibu sana na Bw. Kajela wakimfuatilia.



Katika uchunguzi uliofanywa na watu wa NMB ulibaini kuwa akaunti hiyo ni ya Bi. Hawa Mwarwanda ambaye ni mkazi wa kijijini hapo, na kwammba anahusika katika tukio hilo ambapo mtuhumiwa mwingine naye ilifahamika kuwa ni Bw. Martin Mwarwanda na kwamba ni ndugu wa Bi. Hawa ambapo wote wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano.



Majira ilifanikiwa kuzungumza na Bw. Kajela mlezi wa mtoto huyo, ambaye alisema baada ya kufika katika kituo cha Gapco alimkuta mtoto Boniface na kumuuliza ni nao aliyemteka, mtoto huyo alisema ni fundi wa masofa ambye alikuwa akifanya kazi nyumbani kwake na kwamba alikuwa hajamaliza kazi ya kutengeneza viti hivyo.



"Huyu jamaa sijui kwanini kunitenda hivi kwani ni mtu ambaye kwa vyovyote mtoto asingeweza kutomtambua kwani ni fundi wangu anafanya kazi pake nyumbani kwa malipo ambayo hata hivyo namdani kwani kazi bado haijaisha na pesa yote nilishamlipa labda tama ya fedha inamfanya afikirie kufanya mambo kama haya".



Wakati huo huo Bw. Amosi Willson, anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kumteka mtoto ambaye hakutajwa jina mwenye umri wa miaka mnne na kisha kumficha ndani tukio ambalo lilifanyika katika mtaa wa ear port mbeya mjini tukio ambalo lilitokea Mei 16 saa 7 mchana.



Ilidaiwa kuwa taarifa za kufichwa kwa mtoto huyo zilitolewa na wananchi wa eneo hilo ambao walimwona mtuhumiwa akimnunulia biskuti na pipi kisha kutokomea naye kwa mwendo wa haraka jambo ambalo liliwafanywa wananchi hao kumtilia shaka na kutoa taarifa polisi ambapo alitiwa mbaloni na kwamba watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani mara uchunguzi utakapo kamilika.



Kamanda Nyombi alisema,kutokana na mnatukio hayo,wazazi wanatakiwa kuwa makini na kuwalinda wqatoto wao kwani vitendo vya utekaji watoto umekuwa ukishamiri na kwamba kila mtu anawe mlindi wa watoto wake na kuwazuia watoto hao kupokea vitu kwa watu ovyo.



Mwisho.