WANANCHI wa kata Igurisi wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya wametakiwa kuhakikisha wanapambana na wahalifu kupitia sera ya polisi jamii na ulinzi shirikishi katika maeneo yao ya makazi yao, badala ya kusubiri serikali.
Rai hiyo imetolewa na mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya hiyo, ambaye ni diwani wa kata ya Igurusi BW.Keneth Ndingo, wakati akikabidhi vifaa vya ujenzi na ulinzi kwa vijiji sita vya kata hiyo,Bw.Ndingo alisema kuwa kuendelea kuwa tegemezi pasipo kupambana na wahalifu ambao wengi wanaishi maeneo yanayofahamika ni kosa kwa jamii na kwamba wanapaswa kupambana na tabia ya kulindana kwa kuogopa kuwa mhalifu ni mtoto wa fulani.
Alisema jeshi la polisi bila kuwepo kwa Polisi jamii na ulinzi shirikishi haliwezi kufanya kazi ya kulinda raia na mali zao zaidi ya kubakia lawama ambazo zinaigawa serikali ,chama na watendaji wake na kuwapa nafasi wahalifu kuendelea krwanyanyasa wanamchi
Katika hafla hiyo fupi Bw. Ndingo alikabidhi mabati 180 kwa viongozi wa madhehebu ya kidini katika kata hiyo na kutoa fedha za kujengea ofisi katika vijiji husika
Aidha aliwataka viongozi wa serikali za vijiji kusimamia sheria ndogo za kusimamia ulinzi katika kipindi cha shughuli za uvunaji wa zao la mpunga ambapo kuna kundi la watu wachache hutumia mbinu mbalimbali ili kufanikisha adhma ya kuwaibia mazao wananchi, na kutoa vitisho vya kuwazuia wananchi hao washindwe kulinda mazao kwa madai kuwa kuna wauawaji mashambani na kusababisha hofu ili wao wapate upenyo wa kujichukulia mazao kirahisi.
"kuweni makini na watu wanaozua hofu na kuwaibia mazao yenu vitendo viovu visiachwe na kushamili kupitia kwa wachache wasioipenda nchi kuendelea kuwa na amani na utulivu hasa uchaguzi mkuu wa rais,wabunge na madiwani.
Alisema Ifahamike kwamba serikali inahakikisha usalama wa wananchi wake mali zao, na kuwataka kuepukana na dhana potofu kuwa serikali inawaacha wahalifu waendelee kuwaaibia wananchi mali zao, ambapo alikemea wananchi wenye tabia ya kuwaficha wahalifu na kwamba jambo hilo linasababisha wahalifu kuendelea kufanya watakavyo kwani kuna watu ambao wanawalinda nyuma yao.
Akishukuru kwa niaba ya wananchi waliohudhuria hafra hiyo, Mch. Weston Mwashambwa, wa kanisa la Moravian Igurusi, alishukuru kwa kupatiwa vifaa hivyo na kwamba katika kipindi hiki cha mavuno vitasaidia kupambana na uhalifu kwani kila mwaka huzuka uhalifu ambao unasababisha hasara kwa wakulima baada ya kibiwa mazao yao.
Mch.Mwashambwa alisema, pia katika kiipindi hiki wananchi na hata waumini hukumbwa na hofu baada ya uvumi kutokea kuwa kunawauaji ambao wanafanya mashambani na kusababisha hofu ya kuendelea kulinda mazao yao na kurudi majumbani ambapo wahalifu hutumiwa mwanya huo kuiba mazao na kwamba uvumi huo huanzishwa na wahalifu wenyewe kuwatishia wananchi waache kulinda mali zo shambani.
Mwisho.