SEKTA ya afya wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya,inakabiliwa na changamoto nyingi zikiwepo upungufu wa wauguzi, kukosekana kwa vyoo,maji na vitendea kazi katika wodi.Jambo linalopunguza utendaji wa kazi.
Hayo yamo katika risala iliyosomwa na muuguzi Bi.Rehema Nangali,Katika maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani na kumbukumbu ya mwanzilishi wa kwanza huduma ya uuguzi Bi.Florence Nightngale ,Aliyezaliwa mwaka 1820 na kufariki Agosti 13-1910.
Wauguzi hao wamesema changamoto hizo zinatokana na kuwepo kwa wauguzi waliosajiliwa 64,kati ya 27 waasio wasio wa serikali kutoka 4 mwaka 1999 bila kujali ongezeko la wagonjwa jambo linalopelekea lawama kwao kutoka na kazi zao wakati mwingine kufanywa na wasio na sifa.
Upande wake mganga mkuu wa wilaya Dr.Somoka Nkaran Mwakaopala,amesema idara yake ina upungufu wa watumishi 140 kati ya 344 wanaohitajika na hivyo kuiomba serikali kutatua kero hiyo ili wananchi wapatiwe huduma bora na siyo bora huduma.
Akiwahutubia wakazi wa Mbarali mjini Rujewa aliyekuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo,ambaye ndiye mwenyekiti wa halmashauri Mh.Keneth Ndingo,alisema mkakati wa makusudi unahitajika kuboresha miundo mbinu ,kujenga nyumba za wauguzi,yenye sifa muhimu,ambapo aliwataka kutoangalia maslahi yao bali aliwaasa wafanye kazi kwa bidii wakati serikali inashughulikia matatizo yao.
Bw.Ndingo alisema pamoja na sekta hiyo ya afya kuwa na changamoto nyingi haiwapasi wauguzi kulipiza kisasi kwa wanaowahudumia kwakuwa matatizo mengi yanayowakabili kiutendaji serikali inaendelea kuyatafutia ufumbuzi ili kuleta uwiano kimaslahi.
Alisema serikali inatambua wajibu wake kwa watumishi wa sekta hiyo na nyingine na hivyo kuwataka kuwa na uvumilivu na subira huku wakiendelea kuchapa kazi kwa bidii katika kuwahudumia wananchi ambao tegemeo lao kubwa la kupata huduma ni watumishi.
Mwisho.